Sports

MABORESHO ya Kanuni Za Ligi Kuu ya NBC 2025/2026

MABORESHO ya Kanuni Za Ligi Kuu ya NBC 2025/2026

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepitia na kufanya marekebisho muhimu ya kanuni zitakazotumika kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026. Maboresho haya yamelenga kuongeza ushindani, uwajibikaji, na ubora wa ligi. Hapa chini tumekuandalia muhtasari wa mabadiliko makuu:

1.Kanuni ya 62 – Wachezaji wa Kigeni (Kipengele 1.2)

Klabu hairuhusiwi kusajili zaidi ya golikipa mmoja wa kigeni kwa mashindano yote yaliyo chini ya TFF. Hatua hii inalenga kudhibiti ubora na usawa wa ligi kwa kuhakikisha nafasi ya mlinda mlango inapewa kipaumbele kwa vipaji vya ndani.

2.Kanuni ya 39 – Waamuzi (Kipengele 7.1)

Kamati ya Waamuzi ya TFF sasa inaweza kupanga waamuzi kutoka nje ya Tanzania kusimamia michezo ya Ligi Kuu ya NBC. Lengo ni kuongeza uwajibikaji na ubora wa uchezeshaji kwa kuleta waamuzi wenye uzoefu wa kimataifa.

3.Kanuni ya 41 – Udhibiti wa Wachezaji

Mchezaji atakayepokea kadi ya njano kwenye michezo minne (4) hataruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuata wa timu yake. Awali, adhabu hii ilitolewa baada ya kadi tatu pekee. Sasa imesogezwa hadi nne, ikiongeza nidhamu na kuwapa wachezaji nafasi ya kucheza kwa uwangalifu zaidi.

4.Kanuni ya 08 – Mshindi (Bingwa)

Endapo timu zitamaliza zikiwa na pointi sawa, bingwa atapatikana kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo kwa mpangilio: Mchakato wa kutambua mshindi endapo timu zitalingana pointi:

Timu yenye wastani bora katika matokeo ya michezo iliyozikutanisha timu hizo (Head to Head).

Endapo bado zitalingana, timu yenye tofauti bora ya magoli. Ikiwa bado zitalingana, timu iliyofunga magoli mengi zaidi.

Ikiwa bado zitalingana, timu iliyofungwa mabao machache zaidi. Ikiwa bado zitalingana, timu iliyoshinda michezo ya ugenini nyingi zaidi.

Maboresho: Vimewekwa vigezo vingi vya uwiano (tiebreakers) kuhakikisha mshindi anatambuliwa kwa uwazi.

5.Kanuni ya 17 – Taratibu za Mchezo

Timu zinaruhusiwa kutumia vyumba vya kuvalia (Dressing Rooms) saa 8 kabla ya mchezo kuanza. Timu itakayoshindwa kutekeleza kanuni hii itafungiwa kutumia uwanja wake wa nyumbani kwa michezo isiyopungua mitatu.

Leave a Comment